- Get link
- X
- Other Apps
Top Stories
- Get link
- X
- Other Apps
Ally Kamwe
Young Africans (Yanga SC) watakutana na Gaborone United katika mechi ya marudiano ya Raundi ya Kwanza ya kufuzu CAF Champions League, Jumamosi, Septemba 12, 2026, saa moja usiku (19:00 EAT), kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Mechi hiyo inakuja ikiwa timu hizo zimetoka sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa Botswana, hivyo alama ya jumla kabla ya marudiano ni 1-1. Yanga sasa itahitaji kufanya vizuri katika mchezo huo ili kusonga mbele katika hatua inayofuata.
Yanga inatakiwa kuwa makini hasa kwenye mipira ya kusimama. Msemaji wa klabu Ally Kamwe amesema mechi si rahisi, lakini pia si ya kutisha, huku akisisitiza umuhimu wa kuwa makini tangu mwanzo ili kuzuia madhara yanayoweza kusababishwa na set pieces za wapinzani.
Yanga pia inasubiri kurejea kwa Dickson Job na Clement Mzize,waliofanya vipimo vya kitabibu Afrika Kusini. Timu ya madaktari imethibitisha kuwa wapo salama na wanajiandaa kurejea uwanjani kurejea kwao kunaweza kuwa kama kuwasili kwa usajili mpya.
Siku ya mechi pia imetengwa maalum kama “Sele Day” kwa ajili ya kumkaribisha na kumshangilia Selemani Mwalimu kwa mchango wake wa kimpira huko Botswana. Tiketi zinapatikana kupitia N-Card, huku asilimia 60 ya tiketi za VIP A zikiwa tayari zimenunuliwa. Klabu imewaita mashabiki kujitokeza Azam Complex kuwapa nguvu wachezaji katika mchezo huo.


Comments
Post a Comment