Real Madrid imeshinda mabao 4-1 dhidi ya Sevilla kwenye uwanja wa Santiago Bernabéu, katika mzunguko wa tisa wa LaLiga, Jumapili usiku, Oktoba 18, 2026. Mbappé alifunga mara mbili, lakini jina lililobaki midomoni mwa mashabiki ni la Yan Diomande.
Madrid ilianza kwa kumiliki mpira na kuusogeza mbele mashambulizi. Dakika ya 30, Diomande alianzisha shambulizi lililoishia kwa Arda Güler kufunga bao la kwanza. Dakika saba baadaye, Jude Bellingham alimpa Kylian Mbappé pasi safi, na mshambuliaji huyo akaweka bao la pili kutoka karibu na lango. Huku Madrid ikiingia mapumzikoni kwa uongozi wa mabao 2-0.
Kipindi cha pili kilimpa Mbappé nafasi ya kuandika bao tena. Kwa mkwaju wa penalti, dakika ya 63, shuti kali lililopanda katikati ya lango. Mchezo ulionekana kuwa mgumu kwa wapinzani wao kwa idadi kubwa ya magoli ikiwaondolea utulivu kiwanjanui.
Sevilla ilijaribu kupumua. Dakika ya 80, Manu Bueno alimalizia pasi ya Lucas Stassin na kupunguza pengo hadi 3-1. Matumaini hayo yalidumu dakika mbili tu. Diomande alipokea mpira upande wa kulia kufuatia pasi ya Aurélien Tchouaméni, kisha akapiga shuti lililotua wavuni kuogeza idadi ya mabao kufikia 4-1, dakika ya 82.
Diomande hakuwa mfungaji wa kwanza wala jina kubwa zaidi uwanjani, lakini alikuwa injini ya kila awamu. Alianzisha bao la kwanza, akafunga goli la mwisho, hata hivyo alionekana sana kwenye maeneo sahih, akiisukuma timu mbele kila walipohitaji kufanya mashambulizi. Alipasi vizuri, alirudi kukaba na kurejesha mpira.
Madrid ilitawala mchezo. Ikimiliki zaidi kwa 65% dhidi ya 35%, pia ikipiga pasi nyingi zaidi, na kufika katika eneo la hatari. Tofauti ya ubora ilionekana kwa nafasi kubwa Madrid ilitumia nafasi zake kuzalisha mabao wakati Sevilla ikikosa matumizi ya nafasi zake. Golikipa Thibaut Courtois alikuwa imara alipohitajika, huku Odysseas Vlachodimos akishindwa kuiokoa timu yake pindi Madrid ilipopata nafasi.
Mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa. Dean Huijsen na Félix Correia walionywa dakika ya 23 baada ya mzozo, kisha Juan Iglesias na Marc Cucurella wakapewa kadi za njano baadaye. Penalti ya Mbappé ilitokana na kosa la Andrés Castrin.
Ushindi huu unaonyesha kikosi kinachopata mabao kutoka sehemu tofauti za uwanja: kiungo, pembeni na mbele. Mbappé anaendelea kuwa mfungaji wa kutegemewa, lakini usiku huu ulionyesha kwamba mzigo hauko kwake peke yake. Huku Sevilla, bao la Bueno likikiwa faraja ndogo kwenye mchezo ambao walizidiwa karibu kila eneo la uwanja.







Comments
Post a Comment