Top Stories

CAF na Orodha ya Vilabu Bora Afrika 2026/27

CAF na Orodha ya Vilabu Bora Afrika 2026/27

Shirikisho la Soka Barani Africa (CAF) limetoa viwango vipya vya ubora wa vilabu kwa msimu wa 2026/27, huku Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ikiendelea kushika nafasi ya kwanza baada ya mafanikio yake katika mashindano ya bara.

Vilabu 10 Bora Afrika kwa Mujibu wa CAF 2026/27

1. Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) – Alama 73

2. Al Ahly (Misri) – Alama 66

3. EspĂ©rance (Tunisia) – Alama 58

4. RS Berkane (Morocco) – Alama 57

5. USM Alger (Algeria) – Alama 52

6. Zamalek (Misri) – Alama 49

7. Pyramids (Misri) – Alama 48

8. AS FAR (Morocco) – Alama 41

9. Al Hilal (Sudan) – Alama 39

10, CR Belouizdad (Algeria) – Alama 38

Kwa upande wa Afrika Mashariki, Simba SC ndiyo klabu iliyoshika nafasi ya juu zaidi ikiwa ya 11 kwa alama 38, huku Young Africans (Yanga) ikifuatia katika nafasi ya 12 ikiwa na alama 35. Hali hiyo inaonyesha ushindani unaozidi kuimarika wa vilabu vya ukanda huo katika mashindano ya CAF.

Kwa ujumla, orodha hiyo inaendelea kuonyesha ubora wa vilabu vya Afrika Kaskazini katika michuano ya bara, huku Afrika Kusini ikiendelea kuwa na mwakilishi wake kileleni kupitia Mamelodi Sundowns. Wakati huohuo, vilabu kutoka Afrika Mashariki vinaendelea kupanda katika viwango hivyo kutokana na matokeo yao ya misimu ya karibuni.

Viwango vya CAF vinatokana na matokeo ya vilabu katika mashindano ya kimataifa ya shirikisho hilo kwa misimu iliyopita na hutumika kupima ubora wa timu pamoja na kusaidia katika upangaji wa baadhi ya mashindano ya CAF.

Comments