- Get link
- X
- Other Apps
Top Stories
- Get link
- X
- Other Apps
Simba SC kesho, Jumatano Septemba 16, itashuka dimbani dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex, huku Kocha Mkuu Steve Barker akitambua ukubwa wa kibarua kilicho mbele yao.
Barker amesema mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa Azam, lakini maandalizi ya Simba yameenda vizuri na kikosi chake kiko tayari kupambana hadi dakika ya mwisho kwa lengo la kuondoka na alama tatu.
Kocha huyo amerejea pia kwenye matokeo ya msimu uliopita, ambapo Simba ilikusanya alama moja pekee katika michezo yake dhidi ya Azam. Kwa Barker, hilo ni jambo ambalo hawataki kulirudia katika msimu huu, hasa wakati timu ikiwa imeanza ligi kwa mwendo mzuri.
Rekodi ya mikutano yao ya karibuni inaonyesha ushindani huo. Katika mechi tano zilizopita, Simba imeshinda mara moja, Azam imeshinda mara mbili, huku michezo miwili ikimalizika kwa sare. Hiyo inaifanya safari ya Simba kwenda Azam Complex kuwa nyingine ya kuhitaji umakini mkubwa.
“ Msimu uliopita tulipata alama moja tu dhidi ya Azam, na hiyo ilikuwa ni miongoni mwa changamoto kwenye mbio zetu za ubingwa,”
Barker amesema, akisisitiza kuwa safari hii malengo yao ni kupata alama zote tatu.
Kwa upande wa wachezaji, beki wa kulia Nathaniel Chilambo amesema wanajua wanakwenda kukutana na timu yenye wachezaji imara na benchi la ufundi lenye uwezo, lakini hilo haliwapunguzii kiu yao ya ushindi. Amesema wachezaji wote wamejiandaa kujitoa kwa asilimia 100.
Mchezo wa kesho unaipa Simba nafasi ya kuonyesha kama safari hii inaweza kubadilisha mwenendo wake dhidi ya Azam. Huku wenyeji watakuwa na jukumu la kuonesha ushindani dhidi ya Simba katika pambano ambalo linatarajiwa kuwa miongoni mwa michezo michezo migumu ya ligi kuu.
Matukio ya picha mchezo uliopita wa Simba vs Azam FC





Comments
Post a Comment