Top Stories

SIMBA VS MIGHTY WANDERERS: JE, SIMBA IKO TAYARI KUMALIZA KAZI UHURU?

Simba vs Mighty
Saa 16:00 pm-Uhuru Stadium 

Simba imerudi Dar es Salaam ikiwa na faida ya bao 1-0 kutoka mchezo wa kwanza dhidi ya Mighty Wanderers, safari hii ikiwa na nafasi ya kumalizia kazi mbele ya mashabiki wake katika Uwanja wa Uhuru. Ushindi huo wa Malawi umeiweka Simba kwenye nafasi nzuri, lakini bado kuna dakika 90 zinazohitaji umakini kabla ya tiketi ya hatua inayofuata kuthibitishwa.

Kcha wa Simba SCSteve Barker

Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker, amesema timu yake inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na lengo la kupata ushindi, huku akisisitiza umuhimu wa kucheza kwa morali kubwa mbele ya mashabiki wa nyumbani. Barker amesema:“Ni muhimu kwetu kuingia uwanjani tukiwa na morali ya hali ya juu, tuna mazingira mazuri ya kupata matokeo chanya kwakuwa tunacheza nyumbani mbele ya mashabiki wetu ambao tunaamini watakuja kwa wingi kutupa sapoti.”

Kauli hiyo inaendana na hali ya Simba kuelekea mchezo. Mbali na kucheza Dar es Salaam, timu hiyo inaingia ikiwa tayari imepata matokeo inayoyataka kwenye mchezo wa kwanza. Wakati Wanderers wakilazimika kutafuta namna ya kugeuza bao hilo, Simba inaweza kutumia presha hiyo kucheza kwa mpango na kutafuta bao litakaloweka mambo katika nafasi salama zaidi.

Libasse GuèyeLibasse Guèye

Kikosi pia kimepata ingizo muhimu. Libasse Guèye, ambaye hakuwapo kwenye mchezo wa kwanza kutokana na adhabu ya kadi nyekundu, amerejea kwenye mpango wa timu baada ya kumaliza adhabu yake. uwepo wake pamoja na Anicet Oura, Elie Mpanzu na Clatous Chama ambapo kurejea kwa Guèye kunaongeza chaguo la Simba katika eneo la mbele, hasa katika mchezo ambao Wanderers wanahitaji kutoka kwenye mpango wao wa kujilinda

Mighty Wanderers yenyewe haina nafasi kubwa ya kusubiri. Bao moja iliyo nyuma linawalazimisha kutafuta njia ya kufunga, na hilo linaweza kuufanya mchezo uwe wazi zaidi kadiri muda unavyokwenda. Simba inaweza kutumia nafasi hizo kushambulia, lakini itahitaji pia kuwa makini wasije kuruhusu bao la mapema ambalo linaweza kuibadilishia kabisa presha ya mchezo.

Simba vs Mighty

Faida ya bao moja inaweza kuwa msaada mkubwa, lakini inaweza pia kuwa mtego kama timu itaingia ikiwa na mawazo ya kulinda matokeo pekee. Kushindwa kutumia nafasi za kufunga au kupoteza umakini kwenye maeneo ya nyuma kunaweza kuifanya Simba ijikute ikicheza chini ya presha ambayo wangeweza kuiepuka.

Historia pia iko upande wa Simba inapocheza nyumbani katika michuano hii. Klabu inakumbukumbu nzuri dhidi ya timu za Malawi kwanamna yoyote itataka kutumia uzoefu huo pamoja na mazingira ya nyumbani kumalizia kazi iliyoianza ugenini. Lakini historia pekee haitoshi kazi ya leo itahitaji Simba kucheza kwa utulivu, kutumia nafasi na kudhibiti mchezo.

Dakika 90 za mchezo zitaamua jibu la swali hili, ni kiasi gani Mnyama Simba alikuwa tayari kumaliza kazi katika ndimba la Uhuru.

Comments