Top Stories

GABORONE UNITED vs YANGA LEO: NANI ATAANZA KWA KISHINDO?

GABORONE UNITED vs YANGA

Kocha mkuu wa Yanga SC
Manqoba Mngqithi - Kocha mkuu Yanga SC

Ni siku ya kuanza safari mpya ya Yanga katika anga la Afrika. Mabingwa hao wa Tanzania leo, Jumamosi, Septemba 5, 2026, watakuwa ugenini Botswana kukabiliana na Gaborone United katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza ya Preliminary Round ya CAF Champions League, utakaopigwa Gaborone National Stadium kuanzia saa 8:00 usiku kwa saa za Tanzania.


Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na mwenendo mzuri katika Ligi Kuu ya NBC, ikiwa imeshinda michezo yake yote ya hivi karibuni na kuonyesha kiwango kinachotoa matumaini kuelekea mtihani huu wa kimataifa. Huo ndio msingi ambao kikosi cha Manqoba Mngqithi kinataka kuutumia kuanza vizuri safari ya kusaka nafasi ya kusonga mbele.

Zizo Ki na Shalulile wa Yanga kwenye mazoezi

Macho pia yatakuwa kwa baadhi ya nyota wenye uzoefu walioongezwa kwenye kikosi. Stephane Aziz Ki amerudi Jangwani akiwa tayari anaifahamu vizuri timu na mazingira ya mashindano ya Afrika, huku Peter Shalulile akileta uzoefu mkubwa kutoka Mamelodi Sundowns, ambako alicheza kwa mafanikio makubwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Goborone vs Yanga kwenye CAF CHAMPION leo

Gaborone United, wenyeji wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa wametoka kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Prisons XI katika mchezo wao wa kwanza wa msimu wa Botswana. Hivyo, Yanga inatarajiwa kukutana na timu iliyoanza msimu kwa matokeo mazuri, huku lengo la wageni likiwa kutafuta matokeo chanya Botswana ili kujiwekea msingi mzuri kabla ya mchezo wa marudiano Tanzania.



Comments