Top Stories

CLEMENT MZIZE KUREJEA KIKOSINI - YANGA

Clement Mzize

Clement Mzize
Clement Mzize

Mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize, ameanza hatua nyingine muhimu katika safari yake ya kurejea kwenye ushindani baada ya klabu kuthibitisha kurejea kwake, baada ya kipindi kirefu cha kuwa nje kutokana na jeraha.

Mzize amekuwa nje kwa muda akipitia mchakato wa matibabu na kurejesha utimamu wake, hali iliyomfanya akose sehemu ya mwanzo wa msimu wa 2026/27. Mshambuliaji huyo alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao Yanga ilitarajia kuwakosa mwanzoni mwa kampeni kutokana na majeraha.

Taarifa ya Septemba 9 ilieleza kuwa Mzize pamoja na beki Dickson Job walifanyiwa vipimo vya kina na kuruhusiwa kuanza mchakato wa kurejea baada ya idara ya matibabu ya Yanga kuridhishwa na taarifa hiyo.

Hatua hiyo inampa kocha Manqoba Mngqithi matumaini ya kuongeza tena chaguo kwenye safu yake ya ushambuliaji kadri Mzize anavyoendelea kurejesha utimamu wa mwili. Mshambuliaji huyo anajulikana kwa kasi, movement na uwezo wa kuwasumbua mabeki, sifa ambazo zinaweza kuwa muhimu katika mfumo wa Yanga.

Clement Mzize

Yanga inacheza leo dhidi ya Geita Gold katikati uwanja wa KMC Complex kikosi rasmi kinasubiriwa huenda nyota huyo akajumuishwa  kikosini kutokana na jeraha lake anaweza kupata dakika chache katika michezo ya mwanzo kuruhusu mwili kuanza kupokea ushindani wa kuwania mpira uwanjani.

Mpango wa mazoezi na urejeshaji wa utimamu chini ya uangalizi wa timu ya matibabu na benchi la ufundi. Kadri atakavyokaribia utayari kamili, ndivyo nafasi ya kurejea kwenye kikosi cha ushindani itakavyokuwa kubwa zaidi.


Mzize anarejea uwanjani, huku maendeleo yake yakitoa matumaini ya kumuona tena kwenye kikosi cha Yanga katika michezo ijayo.

Comments