- Get link
- X
- Other Apps
Top Stories
- Get link
- X
- Other Apps
Kiungo wa Bayern Munich, Jamal Musiala, ameanza tena mazoezi baada ya tukio la kuanguka uwanjani katika mchezo wa kirafiki dhidi ya RB Leipzig, huku taarifa mpya zikionyesha kuwa hali yake inaendelea vizuri.
Musiala alianguka muda mfupi baada ya kufunga bao katika ushindi wa Bayern wa 3-1 dhidi ya Leipzig. Alionekana kupoteza mwelekeo kabla ya Ismael Saibari kumdaka na kumzuia kuanguka moja kwa moja chini. Baada ya kupata msaada wa madaktari.
Taarifa mpya ya leo, Agosti 18, inaeleza kuwa Musiala amerejea kwenye uwanja wa mazoezi wa Bayern, lakini bado hajafanya mazoezi pamoja na kikosi kizima. Amefanya mazoezi binafsi yaliyohusisha kazi za mpira, ikiwemo dribbling na upigaji wa mashuti, huku akionekana kuendelea vizuri.
Bayern Munich bado haijatoa taarifa ya kina kuhusu kilichosababisha Musiala kuanguka. Baada ya mchezo dhidi ya Leipzig, mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Max Eberl, alisema Musiala alikuwa anaendelea vizuri, huku ripoti za awali zikihusisha tukio hilo na athari za joto kali wakati wa mchezo.
Musiala anaendelea kufuatiliwa huku akijenga utimamu wake kupitia mazoezi binafsi. Bayern pia inajiandaa kwa mchezo wake wa German Super Cup dhidi ya Borussia Dortmund, lakini bado haijathibitisha iwapo Musiala atakuwa tayari kushiriki katika mchezo huo.

Comments
Post a Comment