- Get link
- X
- Other Apps
Top Stories
- Get link
- X
- Other Apps
Mshambuliaji wa Angola, Depú, ameaga klabu ya Yanga na kurejea katika klabu yake ya zamani, Petro de Luanda. Uamuzi huo unafuatia taarifa ya Petro de Luanda iliyotolewa siku nne zilizopita, ikimtangaza mchezaji huyo kurejea katika klabu hiyo.
Depú amekuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichoshinda Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2025/26. Baada ya kuondoka, mchezaji huyo amechapisha ujumbe wa kuaga kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, akiwashukuru mashabiki wa Yanga na wachezaji wenzake kwa muda aliokuwa nao ndani ya klabu hiyo.
Amesema, “Kwanza, napenda kuwashukuru mashabiki wote wa Yanga kwa mapokezi ya makubwa na kwa sapoti yote waliyonipa. Kwa wenzangu, asanteni sana kwa kila kitu. Ilikuwa furaha kushiriki nanyi. Kila mmoja atabaki kwenye kumbukumbu yangu. Ninajisikia mwenye shukrani sana kwa kila kitu. Huu si kwaheri, bali ni tutaonana.”
Petro de Luanda imemkaribisha tena Depú kwa ujumbe mfupi uliowekwa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ukisema, “De volta ao lugar onde é feliz. Bem-vindo, Depú!” Ujumbe huo una maana ya “Amerudi mahali anapofurahia. Karibu tena, Depú,” ukithibitisha kurejea kwa mshambuliaji huyo katika klabu yake ya zamani.

Comments
Post a Comment