- Get link
- X
- Other Apps
Top Stories
- Get link
- X
- Other Apps
Al Nassr imefanya comeback kubwa na kuifunga Al Ettifaq 3-2 katika mchezo wa raundi ya tatu ya Saudi Pro League, baada ya kwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa mabao 2-0.
Al Ettifaq ilipata mabao kupitia Ondrej Duda dakika ya 31 na Álvaro Medrán dakika ya 45+3, ikiingia mapumziko ikiwa na faida ya mabao mawili.
Al Nassr ilianza kurejea kipindi cha pili kupitia Sadio Mané dakika ya 74, kabla Abdulelah Al-Amri kusawazisha dakika ya 77.
Mchezo ulionekana kuelekea sare, lakini Mané akatokea tena katika dakika za nyongeza na kufunga bao la tatu, akakamilisha ushindi wa Al Nassr wa 3-2.
Al Nassr, kwa ushindi huu una uzito zaidi kutokana na namna ulivyopatikana timu ikiwa nyuma kwa mabao mawili, kisha ikafunga mabao matatu kipindi cha pili na kuondoka na pointi zote.

Comments
Post a Comment