- Get link
- X
- Other Apps
Top Stories
- Get link
- X
- Other Apps
Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026 yanakwenda ukingoni nchini Morocco, huku timu nne zilizofika hatua ya mwisho zikitarajiwa kucheza ndani ya siku mbili zijazo.
Morocco na Algeria zitakutana katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu utakaochezwa Jumamosi, Agosti 15, 2026. Morocco ilikosa nafasi ya fainali baada ya kutolewa na Cameroon kwa mikwaju ya penalti, huku Algeria nayo ikipoteza dhidi ya Malawi kwa mabao 3-1 katika hatua ya nusu fainali.
Mchezo huo utatoa nafasi kwa timu hizo mbili kumaliza mashindano kwa kushika nafasi ya tatu barani Afrika, baada ya kushindwa kufuzu kwa mchezo wa kuwania ubingwa.
Kwa upande mwingine, macho yote yataelekezwa kwenye fainali ya WAFCON 2026 kati ya Malawi na Cameroon, itakayochezwa Jumapili, Agosti 16, 2026, mjini Rabat. Malawi imefanya historia kwa kufika fainali katika ushiriki wake wa kwanza wa mashindano hayo, huku Cameroon ikifika fainali kwa mara ya nne ikiwa bado inatafuta taji lake la kwanza la WAFCON.
Hatua mbili za mwisho za WAFCON 2026 zitatoa majibu mawili muhimu, Morocco au Algeria itaondoshwa na nafasi ya tatu, kabla ya Malawi na Cameroon kukutana katika pambano la mwisho la kuamua bingwa wa Afrika kwa upande wa wanawake.

Comments
Post a Comment