Top Stories

Mshambuliaji aliyetikisa Yanga Day, Simba yamuweka kwenye rada

Toni Talasi kuja Simba mbadala wa mwalimu

Tonny Talasi, mshambuliaji mwenye miaka 20 wa Les Aigles du Congo, ameanza kuvuta macho baada ya kuifunga Yanga mabao mawili kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi Agosti 9, 2026.

Talasi alifunga mabao yote ya Les Aigles du Congo katika ushindi wa 2 -1 dhidi ya Yanga, akionyesha utulivu mbele ya lango, uwezo wa kucheza na wenzake na kufanya mikimbio hatari ndani ya boksi.

Mshambuliaji huyo pia ni sehemu ya timu ya taifa ya Congo U20, akiwa katika hatua ya mwanzo ya safari yake ya soka lakini tayari akionyesha uwezo wa kucheza katika kiwango cha ushindani.

Jina la Talasi sasa linaingia kwenye picha wakati Simba ikiendelea kuongeza chaguo katika safu yake ya ushambuliaji. Klabu hiyo tayari imefanya usajili wa Ibrahim Doumbia kutoka AS Korofina kuelekea msimu mpya.

Kwa Talasi, kilichoongeza mvuto wake ni kile alichokifanya dhidi ya Yanga. Mabao mawili katika mchezo huo.

Comments