- Get link
- X
- Other Apps
Top Stories
- Get link
- X
- Other Apps
Klabu ya Trabzonspor ya Uturuki imethibitisha rasmi kuwa imeanza mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Misri, Mohamed Salah, katika hatua inayoweza kuwa moja ya usajili mkubwa zaidi wa dirisha hili la usajili.
Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao yake ya kijamii, Trabzonspor imesema Salah anatarajiwa kuwasili Istanbul leo kwa ajili ya kuendelea na mazungumzo ya mwisho kuelekea kukamilisha uhamisho wake.
Baada ya hatua hiyo, nyota huyo anatarajiwa kuelekea jijini Trabzon ambako atapokelewa na mashabiki wa klabu hiyo, huku utambulisho wake rasmi ukitarajiwa kufanyika mara baada ya taratibu za mwisho kukamilika.
Salah kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuondoka Liverpool mwishoni mwa mkataba wake, jambo linalofungua mlango wa kujiunga na klabu mpya bila ada ya usajili.
Wakati Trabzonspor imethibitisha kuanza kwa mazungumzo, vyombo mbalimbali vya habari duniani pamoja na mwandishi wa usajili Fabrizio Romano vimeripoti kuwa pande hizo ziko karibu kukamilisha makubaliano ya mkataba wa miaka miwili. Hata hivyo, klabu bado haijatangaza rasmi kuwa usajili huo umekamilika.
Iwapo dili hilo litafungwa rasmi, Salah ataongeza nguvu kubwa katika Ligi Kuu ya Uturuki na kuandika sura mpya ya maisha yake ya soka baada ya kipindi cha mafanikio makubwa akiwa Liverpool.

Comments
Post a Comment