Top Stories

WAFCON 2026: Tanzania kucheza na Afrika Kusini leo katika Kundi B

WAFCON 2026 Tanzania kucheza dhidi ya South Africa Morocco

Tanzania kucheza dhidi ya Afrika Kusini leo katika mchezo wa Kundi B wa Michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2026.

Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Moulay Rachid mjini Casablanca, Morocco.

Tanzania na Afrika Kusini ni miongoni mwa timu nne zilizopangwa Kundi B, pamoja na Cote d'Ivoire na Burkina Faso.

Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano, mchezo wa pili wa Kundi B leo utazikutanisha Cote d'Ivoire na Burkina Faso katika Uwanja wa Larbi Zaouli, Casablanca.

WAFCON 2026 imezikutanisha timu 16 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika zikishindania ubingwa wa wa bara la Africa kwenye ligi ya wanawake.

Baada ya mchezo wa leo, Tanzania itakutana na Burkina Faso kabla ya kuhitimisha hatua ya makundi kwa mchezo dhidi ya Côte d'Ivoire.

Afrika Kusini nayo itaendelea na ratiba ya Kundi B kwa kucheza dhidi ya Cote d'Ivoire kabla ya kumaliza hatua ya makundi kwa mchezo dhidi ya Burkina Faso.

Comments