Top Stories

FIFA yapinga vikali juhudi za kumdhoofisha Gianni Infantino

FIFA yamtetea Infantino dhidi ya juhudi za kumdhoofisha.

FIFA imemtetea Rais wake, Gianni Infantino, ikisema haitakubali mchakato wowote wa uchaguzi wa urais wa taasisi hiyo unaokiuka Katiba, taratibu za kidemokrasia na mfumo wake wa utawala.

Katika taarifa iliyotolewa na FIFA, taasisi hiyo imesema Infantino alichaguliwa kidemokrasia na vyama wanachama vya FIFA na bado anaendelea kuhudumu kwa mamlaka waliyopewa na wanachama hao.

FIFA pia imedai kuwa kuna juhudi zinazoendelea za baadhi ya watu kujaribu kuidhoofisha taasisi hiyo pamoja na Rais wake, kupitia madai, insinuations na taarifa ambazo imezitaja kuwa hazina ushahidi au zinapotosha.

Taasisi hiyo imeongeza kuwa inakaribisha uchunguzi na ukosoaji halali, lakini imeonya dhidi ya kuwasilisha madai ambayo hayajathibitishwa kama ukweli. FIFA imesema pale taarifa zinapokuwa si sahihi au zinapotosha, itazipinga moja kwa moja.

Kwa upande mwingine, FIFA imemtaja Infantino kama kiongozi ambaye ametumia zaidi ya miaka 30 katika soka la Ulaya na dunia, akidai kuwa uongozi wake umechangia mabadiliko katika mchezo huo, ikiwemo kupanua fursa na rasilimali katika maeneo mbalimbali ya dunia.

FIFA imesisitiza kuwa itaendelea kuzingatia majukumu yake kwa vyama wanachama 211 na kuendeleza ajenda yake ya kulifanya soka kuwa la kimataifa zaidi.

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa FIFA, huku taasisi hiyo ikiwa haijawataja kwa majina watu inayodai wanahusika katika juhudi hizo za kumdhoofisha Infantino.

Comments